Home Kaunti Waathiriwa wa shambulizi la bomu Nairobi hawajalipwa fidia, asisitiza Seneta Kavindu

Waathiriwa wa shambulizi la bomu Nairobi hawajalipwa fidia, asisitiza Seneta Kavindu

Seneta wa kaunti ya Machakos Agnes Kavindu
Seneta wa kaunti ya Machakos Agnes Kavindu
Seneta wa kaunti ya Machakos Agnes Kavindu ameishutumu serikali ya Marekani kufuatia kauli zake za hivi karibuni kuwa iliwalipa fidia waathiriwa wa shambulizi la bomu la mwaka 1998 jijini Nairobi.
Kavindu anasema madai kwamba waathiriwa wamelipwa fidia ni ya uongo akiongeza kuwa watu pekee waliolipwa fidia ni wafanyakazi wa ubalozi wa Marekani.
Akizungumza katika mkutano wa kikanda wa wanawake wa kanisa la AIC kwenye chuo cha mafunzo ya Biblia cha Ukamba katika kaunti ya Machakos, Seneta huyo alisisitiza kuwa Kenya haipo vitani na kundi la wanamgambo la Al-Qaeda lakini ilijipata katika vita kati ya kundi hilo na Marekani.
Ikizingatiwa kuwa Marekani ni nchi inayotetea haki za binadamu, Kavindu alisema nchi hiyo inapaswa kuwazingatia waathiriwa wa bomu hilo katika sheria zake za ufadhili dhidi ya ugaidi.
Website | + posts
Jonathan Mutiso
+ posts