Home Biashara Waathiriwa wa mradi wa eneo la kiuchumi la Dongo Kundu kufidiwa

Waathiriwa wa mradi wa eneo la kiuchumi la Dongo Kundu kufidiwa

Mvurya alisema kuwa halmashauri ya bandari nchini, KPA kama shirika la utekelezaji tayari imefadhiliwa kwa shilingi bilioni- 1.4 kuhitimisha mpango wa utoaji fidia kufikia mwezi ujao.

0
Waziri wa Biashara Salim Mvurya, azuru eneo maalum la kiuchumi la Dongo Kundu.
kra

Waziri wa biashara na ustawi wa viwanda Salim Mvurya, amesema shilingi bilioni1.4 zimetengwa kuharakisha shughuli ya kuwafidia watu walioathirika kutokana na ujenzi wa eneo maalum la kiuchumi la Dongo-Kundu.

Akizungumza wakati wa mkutano wa kutathmini ufanisi kwa mashirika ya utekelezaji wa eneo maalum la kiuchumi la la Dongo-Kundu Jijini Mombasa, Mvurya alisema kuwa halmashauri ya bandari nchini, KPA kama shirika la utekelezaji tayari imefadhiliwa kwa shilingi bilioni- 1.4 kuhitimisha mpango wa utoaji fidia kufikia mwezi ujao.

kra

Waziri huyo aliongeza kuwa shughuli hiyo itatekelezwa kwa awamu mbili ambapo  watu 1,648 watapewa ardhi mbadala na kusaidiwa kuimarisha maeneo yao mapya.

Alisema kuwa KPA itatoa uongozi wa zoezi hilo, ili kuhakikisha kwamba shughuli hiyo inatekelezwa bila matatizo yoyote huku pia ikishughulikia malalamishi ya watu hao.

Kulingana na waziri huyo, ardhi iliyotengewa waathiriwa hao ni ya ukubwa wa ekari 430, huku halmashauri ya KPA ikijukumiwa kusimamia shughuli hiyo.

“Miongoni mwa maswala muhimu ni ujenzi wa miundomsingi kama vile barabara,uunganishwaji wa maji na nguvu za umeme,” alisema waziri huyo.

Wengine waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na viongozi kutoka kaunti za Mombasa na Kwale, asasi mbali mbali za serikali, katibu katika idara ya uwekezaji  Abubakar Hassan Abubakar pamoja na mwenyekiti na mkurugenzi mkuu wa halmashauri ya bandari nchini KPA.

Website | + posts