Home Michezo Waaniaji tuzo ya mwanandinga bora Afrika wabainika

Waaniaji tuzo ya mwanandinga bora Afrika wabainika

0

Orodha ya wanandinga wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka barani Afrika mwaka huu imetangazwa.

Baadhi ya walioteuliwa ni pamoja na washindi  wa mwaka uliopita Sadio Mane wa Senegal na Asisat Oshaola wa Nigeria kwa wanaume na wanawake mtawalia.

Wachezaji 30 wameteuliwa kuwania tuzo  kuu ya wanaume ,wengine 20 wanawania tuzo ya mchezaji bora katika mashindano ya vilabu ,kocha bora wa mwaka,Klabu bora ya mwaka na timu bora ya taifa  pamoja na mchezaji chipukizi bora wa mwaka.

Pia kwa mara ya kwanza CAF imeanzisha tuzo ya kipa bora barani Afrika kwa wale wanaosakata  soka Afrika kwa wanaume na wanawake.

Baadhi ya wanandinga  waliojumuishwa katika orodha ya 30 bora wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa kiume wa mwaka ni  Ramy Bensebaini wa Algeria na  klabu ya Borusia Dortmund,Riyad Mahrez wa Algeria na klabu ya  Al Ahli,Edmond Tapsoba  wa Burkina Faso na Bayer Leverkusen ,Andre-Frank Zambo Anguissa  wa Cameroon na SSC Napoli na Vincent Aboubacar  kutoka Cameroon na klabu ya  Besiktas.

Wengine katika orodha ni Mohamed ElShenawy  wa Misri na  Al Ahly ,Thomas Partey wa  Ghana na  Arsenal ,Achraf Hakimi  wa Morocco na  Paris Saint-Germain,Azzedine Ounahi wa Morocco na Olympique Marseill,Hakim Ziyech wa Morocco  na  Galatasaray,Sofyan Amrabat  wa Morocco na  Manchester United na  Victor  Osimhen wa Nigeria na klabu ya Napoli.

Washindi watabainika kwenye halfa itakayoandaliwa mjini Marrakech Morocco Disemba 11.