Home Habari Kuu Wauguzi walaani shambulizi katika hospitali ya Busia

Wauguzi walaani shambulizi katika hospitali ya Busia

0

Chama cha Waauguzi Nchini kimeshutumu kitendo cha kushambuliwa kwa muuguzi aliyekuwa zamuni katika hospitali ya Port Victoria, kaunti ya Busia.

Mwanamke mmoja aliyeandamana na mwanamume walifika hospitalini hapo wakitaka kuhudumiwa haraka na kurusha cheche za matusi huku wakirusha na kutapakaza vitabu vya hospitali.

Rais wa chama cha wauguzi nchini Collins Ajwang, ametaka hatua za kisheria kuchukuliwa dhidi ya mwanamke huyo.

Mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina Vanessa Agema, alisikika kwenye video iliyosambazwa mtandaoni akimtusi muuguzi huyo huku akijihusisha na mwanasiasa mmoja mashuhuri wa eneo hilo.

Waziri wa Afya Susan Nakhumicha jana Alhamisi pia alitaka mwanamke huyo ambaye imebainika ni mwanafunzi wa teknolojia ya upasuaji katika chuo cha Hospitali ya The Nairobi Women’s kuchukuliwa hatua kali.

Website | + posts