Home Kimataifa Vyuo vya TVET kupokea vifaa vya kisasa kutoka serikali ya China

Vyuo vya TVET kupokea vifaa vya kisasa kutoka serikali ya China

Dkt. Muoria, alifafanua kuwa shilingi hizo bilioni 13 zinatolewa kama mkopo kupitia vifaa vinavyojumuisha vile vya kisasa na vya teknolojia ya hali ya juu.

0
katibu katika idara ya vyuo vya mafunzo ya kiufundi TVET Dkt. Esther Thaara Muoria.
kra

Vyuo 70 vya mafunzo ya kiufundi TVET, vitapokea vifaa vya hali ya juu vya thamani ya shilingi bilioni 13 kutoka China, chini ya mpango wa makubaliano wa serikali kwa serikali, unaolenga kuimarisha sekta ya TVET.

Akizungumza na wanahabari katika afisi yake iliyoko jumba la Jogoo jijini Nairobi, katibu katika idara ya vyuo vya mafunzo ya kiufundi TVET Dkt. Esther Thaara Muoria,  alisema mradi wa TVET kati ya Kenya na China, umewadia wakati ufaao, akisisitiza haja ya kuvipa taasisi hizo vifaa vya teknolojia ya juu.

kra

Dkt. Muoria, alifafanua kuwa shilingi hizo bilioni 13 zinatolewa kama mkopo kupitia vifaa vinavyojumuisha vile vya kisasa na vya teknolojia ya hali ya juu.

Vifaa hivyo vitasambazwa katika idara zote za TVET, ikiwa ni pamoja na idara ya mashini za kilimo, usimamizi wa hoteli, magari na umeme.

Katibu huyo aliishukuru serikali kwa kuendelea kuunga mkono sekta ya TVET, akisema Kenya sasa inajivunia kuwa na taasisi 240 za TVET kote nchini.

Website | + posts