Home Michezo Voeller ataeuliwa kocha wa Ujerumani miezi 9 kabla ya fainali za Euro

Voeller ataeuliwa kocha wa Ujerumani miezi 9 kabla ya fainali za Euro

Kibarua cha kwanza kwa Voeller ni mchuano wa kirafiki kati ya Ujerumani dhidi ya Ufaransa Jumanne wiki hii .

0

Ujerumani imemteua Rudi Voeller kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa kuchukua nafasi ya Hansi Flick aliyetimuliwa.

Kibarua cha kwanza kwa Voeller ni mchuano wa kirafiki kati ya Ujerumani dhidi ya Ufaransa Jumanne wiki hii .

Flick alipigwa kalamu kufuatia kipigo cha Ujerumani cha mabao 4-1 nyumbani Jumamosi, iliyopita na Japan na kuendeleza msururu wa matokeo duni ambapo pia kwa mara ya kwanza timu hiyo ilibanduliwa katika hatua ya makundi ya kombe la dunia mwaka uliopita.

Voeller anashika hatamu za kuinoa Ujerumani miezi 9 pekee kabla ya taifa hilo kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la Euro mwaka ujao .