Home Kimataifa Vituo vya ECDE Turkana vyapokea unga wa uji uliorutubishwa

Vituo vya ECDE Turkana vyapokea unga wa uji uliorutubishwa

0
kra

Vituo zaidi ya 1,000 vya chekechea, ECDE katika kaunti ya Turkana vinatazamiwa kufaidika na mifuko 8,333 ya unga wa uji uliorutubishwa wa kilo 25.

Ugavi huo utahusisha Turkana ya Kati itakayotokea mifuko 1,733, Turkana Mashariki mifuko 1000 huku Loima, Turkana Magharibi, na Turkana Kaskazini ikipokea mifuko 1,400 kila moja.

kra

Waziri wa Michezo na Mafunzo ya Ufundi wa serikali ya kaunti ya Turkana Leah Losiru, alisema kuwa programu za lishe shuleni zimeongeza kiwango cha mahudhurio na mpito hasa katika maeneo kame kama vile Turkana.

Unga wa uji uliorutubishwa kwa mchanganyiko wa sukari, mahindi, soya, vitamini na madini muhimu, unatarajiwa kutoa lishe ya thamani ya juu ya kwa wanafunzi wa ECDE.

Mpango huo unaonyesha kujitolea kwa serikali ya kaunti ya Turkana kusaidia elimu ya watoto wachanga na kushughulikia changamoto zinazokabili jamii katika maeneo kame.

Rahab Moraa
+ posts