Home Kimataifa Vita vya Israel Gaza: Mfalme wa Jordan ahimiza kusitishwa kwa mapigano

Vita vya Israel Gaza: Mfalme wa Jordan ahimiza kusitishwa kwa mapigano

0

Mfalme wa Jordan Abdullah II amemwambia Rais wa Marekani Joe Biden kwamba dunia “haiwezi kumudu” mpango wa Israel wa kuvamia Rafah, ambapo zaidi ya watu milioni 1.4 wametafuta hifadhi.

Israel imezua hofu katika eneo la Rafah baada ya kuanza mashambulizi ya angani ambayo yamewaua mamia ya watu huku ikijitayarisha kwa uvamizi wa ardhini.

Hamas imesema mateka watatu zaidi wa Israel wameuawa katika mashambulizi ya Israel katika eneo lililozingirwa la Gaza.

Kwingineko raia wa Israel wamewapiga risasi Wapalestina wawili, kuchoma moto magari na kuharibu mali katika usiku wa ghasia za walowezi katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.

Mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza yamesababisha vifo vya Wapalestina wasiopungua 28,340 na kuwajeruhi wengine 67,984 tangu Oktoba 7. Idadi ya vifo nchini Israel kutokana na mashambulizi ya Oktoba 7 yaliyoongozwa na Hamas ni 1,139.

BBC
+ posts