Israel imewahamisha baadhi ya raia wake kaskazini mwa nchi kuwa lengo rasmi la vita, Ofisi ya Waziri Mkuu imesema.
Uamuzi huo ulifikiwa na Baraza la Mawaziri la Usalama la Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu siku ya Jumatatu.
Takriban watu 60,000 wamehamishwa kutoka kaskazini mwa Israel kutokana na mashambulizi ya karibu kila siku ya kundi la Hezbollah linaloungwa mkono na Iran katika nchi jirani ya Lebanon.
Mapigano ya mpakani yaliongezeka tarehe 8 Oktoba 2023 – siku moja baada ya shambulio baya dhidi ya Israel na wapiganaji wa Hamas kutoka Ukanda wa Gaza – wakati Hezbollah iliposhambulia Israel, kamhatua ya kuunga mkono Wapalestina.
“Baraza la Mawaziri la Usalama limeimarisha malengo ya vita hivyo kujumuisha yafuatayo: Kuwarejesha wakazi wa kaskazini kwa usalama nyumbani kwao,” taarifa kutoka ofisi ya waziri mkuu ilisema.
“Israel itaendelea kuchukua hatua kutekeleza lengo hili,” iliongeza.
Mapema Jumatatu, Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant alisema njia pekee ya kuwarejesha wakazi wa kaskazini mwa Israel kwenye makazi yao ni kupitia “hatua za kijeshi”, wakati wa mkutano na mjumbe wa Marekani Amos Hochstein.