Home Habari Kuu Vita dhidi ya wizi wa mifugo vinazaa matunda, asema Waziri Kindiki

Vita dhidi ya wizi wa mifugo vinazaa matunda, asema Waziri Kindiki

0

Waziri wa Usalama wa Kitaifa Prof. Kithure Kindiki anasema mafanikio makubwa yanazidi kupatikana katika vita vinavyoendelea dhidi ya wezi wa mifugo wanaowahangaisha wakazi wa eneo la kaskazini mwa nchi.

Ili kudhihirisha hilo, Prof. Kindiki leo Alhamisi alikuwa katika eneo la Mulango, kaunti ya Isiolo na kushuhudia kurejeshwa kwa zaidi ya  ngamia 200 walioibwa siku chache zilizopita na kisha kupatikana.

Operesheni ya kuwasaka ngamia hao iliendeshwa na maafisa kutoka kambi ya kikosi cha kukabiliana na wizi wa mifugo ya Mulango, kaunti ya Isiolo.

Waziri Kindiki alielezea kujitolea kwa serikali kutoa mpangokazi wa sera ya kuangamiza uhalifu na kuwazawadia na kuwatia moyo maafisa wa usalama wanaodhihirisha kujitolea kwao katika kukomesha matishio ya uhalifu.

Aidha Waziri alionya kuwa maafisa wa usalama, umma na viongozi wa aina yoyote wanaowezesha uhalifu watakabiliwa vikali kisheria.

Wakati wa hafla ya ukabidhi wa ngamia hao, viongozi wa kisiasa wa kaunti za Isiolo na Samburu walielezea nia yao ya kusaidia katika kuwatambua watu wanaoshukiwa kuendeleza wizi wa mifugo na kuhakikisha mifugo walioibwa wanarejeshwa.

 

 

Website | + posts