Home Kaunti Visa vya unajisi vyashamiri Busia

Visa vya unajisi vyashamiri Busia

0
kra

Kaunti ya Busia imetajwa kuwa niongoni mwa kaunti zilizo na visa vingi vya unajisi.

Haya ni kwa mujibu wa ripoti ya utafiti wa afya na eneo ya mwaka wa 2022.

kra

Ripoti hiyo ilibaini kuwa jumla ya asilimia 14.7 ya wanawake na wasichana wenye umri wa miaka 15-45 ni waathiriwa wa visa hivyo.

Baadhi ya visa hivyo ni kama kile cha mwezi wa Mei mwaka jana ambapo mfanyakazi wa shambani wa mwakilishi wa kaunti (MCA) alipomnajisi msichana wa umri wa miaka 11 aliye pia binamu wa mwakilishi huyo.

Inadaiwa kuwa, Emily alikuwa anacheza na watoto wa mwakilishi huyo nyumbani kwa mwakilishi huyo alipoitwa na mfanyakazi huyo chumbani na kumnajisi.

Akiwa katika tendo hilo, mke wa mwakilishi huyo alimfumania na kumwelekeza mvulana huyo aende shambani mara moja.

Mumewe aliporudi jioni, alimweleza yaliyojiri naye kwa mshangao akamweleza mkewe ampeleke msichana huyo hospitalini bila kuwaeleza wazazi wake.

Hata hivyo, taarifa hiyo ilifichuka baada ya dada mkuu wa Emily aliyekuwa ameenda sokoni kuisikia na kumpasha babake-Ricky aliyekuwa amelala nyumbani akiuguza malaria.

Kwa mshangao, aliamka mara moja na kuelekea eneo la tukio na kumpata mama ya mwakilishi huyo aliyemhakikishia taarifa hiyo ila hakumweleza hospitali aliyopelekwa.

Ricky alipiga ripoti kwa kituo cha polisi na walipokuja kumshika mshukiwa huyo, tayari alikuwa ametoweka.

Ricky alidai kuwa, MCA alijaribu kumhonga shilingi 100,000 kuondokoa kesi hiyo ila akadinda.

Kwa sasa anaomba serikali ifanye hima kumtafuta mvulana huyo ili haki itendeke.

Kisa kingine ni cha bwana Ali ambaye mwanawe wa umri wa miaka 13, alinajisiwa mwaka wa 2019 na mwana wa afisa wa jeshi la ulinzi.

Vile vile, alikat’aa hongo ya shilingi 100,000.

Baadaye, ushaidi wa nguo, malazi na faili ulitoweka kutoka chumba cha uhifadhi kwa njia ya utata huku naye shahidi wa keshi hiyo akijiondoa.

Kwa mujibu wa mzee wa kiji wa eneo hilo- David Ochieng, visa vya watu wenye hela na ushawishi kuvuruga kesi za unajisi vimeshamiri mno.

Alifichua kuwa, tangu aanze kazi hiyo mwaka wa 2018, hupokea kesi nne za unajisi kila mwezi ambazo wazazi na wanafamilia hutaka mazungumzo ya suluhu kufanyika nje ya mahakama ila yeye hukataa na kusisitiza njia ya kotini.

Kufuatia wingi wa visa hivyo, hivi karibuni, hakimu wa mahakama ya Busia alimukumu mwanaume mmoja miaka 30 gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kumnajisi msichana miaka tano na pia kumwambukiza ugonjwa.

Namo septemba mwaka jana, MCA mmoja alifikishwa mahamani kwa kumnajisi msichana wa miaka 14 baada ya maandamo ya wanawake waliolaani kitendo hicho.