Ndoto ya mabingwa watetezi Marekani kushinda Kombe la Dunia la nne kwa mpigo ilizimwa jana Jumapili baada ya kushindwa penalti 4 kwa 5 na Uswidi katika mchuano wa raundi ya 16 bora.
Mechi hiyo iliishia sare tasa baada ya dakika 120 huku kipa wa Uswidi Zecira Musovic akipangua zaidi ya matobwe kumi ya Marekani.
Katika hatua ya penalti, timu zote zilifunga penalti 3 na kupoteza mbili kabla ya Uswidi kufunga penalti ya 6 huku Marekani wakipoteza.
Uswidi watamenyana na Japani katika robo fainali.
Awali, Uholanzi waliilemea Afrika Kusini magoli mawili kwa bila na watachuana na Uhispania katika robo fainali.