Home Michezo Vipusa wa Kenya watua nchini baada ya kuibwaga Burundi

Vipusa wa Kenya watua nchini baada ya kuibwaga Burundi

0

Timu ya taifa ya Kenya kwa wasichana walio chini ya umri wa miaka 17 maarufu kama Rising Starlets, imewasili nyumbani leo Alasiri kutoka Adis Ababa Ethiopia, ilipowashinda Burundi mabao matatu kwa bila Jana katika mechi ya kufuzu kwa kombe la dunia.

Kikosi hicho kimelakiwa na Waziri wa michezo Ababu Namwamba punde kilipowasili katika angatua ya Jomo Kenyatta.

Kenya itawaalika Burundi Jumapili hii kwa mechi ya marudio katika uwanja wa Ulinzi Complex wakihitaji kudumisha ushindi huo, ili kuweka historia kuwa timu ya kwanza ya soka kutoka Kenya kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia.

Fainali za Kombe la Dunia kwa wasichana walio chini ya umri wa miaka 17 ziataandaliwa katika Jamhuri ya Dominika, kuanzia Oktoba 16 hadi Novemba 3 mwaka huu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here