Home Michezo Vipusa wa Kenya wang’atwa nyumbani na Cameroon

Vipusa wa Kenya wang’atwa nyumbani na Cameroon

0

Matumaini ya Timu ya taifa ya Kenya kwa wasichana wasiozidi umri wa miaka 20 kufuzu kwa kombe la dunia mwaka ujao, yamezimwa baada ya kupigwa mabao 3-2 na Cameroon, katika marudio ya mechi ya raundi ya tatu iliyosakatwa Ijumaa katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo.

Cameroon wamefuzu raundi ya nne kwa ushindi wa jumla wa mabao  6-2 baada ya kuicharaza kenya magoli 3-0 katika  mkondo wa kwanza wiki iliyopita mjini Yaiounde Cameroon.

Website | + posts