Home Habari Kuu Viongozi waonywa dhidi ya kuingiza siasa katika maswala ya usalama

Viongozi waonywa dhidi ya kuingiza siasa katika maswala ya usalama

Wakazi wa kaunti ya Lamu wamehimizwa kutoa habari kwa maafisa wa usalama, kuhusu watu wanaoshukiwa kushiriki uhalifu

0
Waziri wa usalama wa kitaifa Prof. Kithure Kindiki akiwa kaunti ya Lamu.

Waziri wa usalama wa kitaifa Prof. Kithure Kindiki amewaonya viongozi waliochaguliwa dhidi ya kuingiza siasa katika maswala ya usalama wa taifa.

Huku akiwapongeza maafisa wa usalama kwa kukabiliana na magaidi, waziri Kindiki alisema asasi za usalama zimefaulu kutibua mashambulizi ya kigaidi yaliyokuwa yamepangwa katika maeneo tofauti katika kaunti ya Lamu, ambapo baadhi ya maafisa wamefariki na wengine kuachwa na majeraha mabaya.

Aliyasema hayo akiwa katika kisiwa cha Pate kaunti ya Lamu, ambako anafanya ziara ya kukadiria hali ya usalama baada ya eneo hilo kushuhudia mashambulizi ya kigaidi.

Ziara hiyo inajiri siku mbili baada ya wanajeshi kadhaa wa Vikosi vya Ulinzi vya Kenya (KDF) waliokuwa wakishika doria, kujeruhiwa baada ya gari lao kukanyaga kilipuzi.

Aidha waziri huyo alifungua rasmi makao makuu ya kaunti-ndogo ya Lamu Mashariki, na kufanya kikao na kamati za usalama na ujasusi za eneo la Pwani, kaunti ya Lamu na kaunti ndogo ya Lamu Mashariki.

Wakazi wa kaunti ya Lamu wamehimizwa kutoa habari kwa maafisa wa usalama, kuhusu watu wanaoshukiwa kushiriki uhalifu katika juhudi za kuimarisha usalama katika eneo hilo.

Website | + posts