Home Habari Kuu Viongozi wahimizwa kuwaheshimu wananchi

Viongozi wahimizwa kuwaheshimu wananchi

Mzee Gikonyo, ambaye alifariki wiki iliopita , alianza kufanya biashara mwaka wa 1930 akiwa mchuuzi jijini Nairobi.

0
Naibu Rais Rigathi Gachagua.
kra

Rais  William Ruto na naibu wake Rigathi Gachagua leo Jumamosi, walitoa heshima zao kwa mfanyabiashara maarufu jijini  Nairobi, Mzee Gerald Gikonyo Kanyuira kwa mchango wake katika sekta ya biashara  na kujitolea kwake kutumikia taifa hili.

Katika taarifa iliyosomwa kwa niaba yake na Naibu Rais Rigathi Gachagua, wakati wa  ibada ya mazishi ya mfanyabiashara Mzee Gerald Gikonyo Kanyuria, eneo la Kangema kaunti ya Murang’a, Rais William Ruto alimuomboleza Mzee Gikonyo akimtaja kuwa atakumbukwa kwa unyenyekevu wake, mwenye maadili na jasiri.

kra

Rais Ruto alisema mzee Gikonyo alijitolea kikamilifu katika biashara, hatua iliyochochea ukuaji wa sekta ya biashara Jijini Nairobi katika enzi za ukoloni.

Kwa upande wake naibu rais Rigathi Gachagua alisema mzee Gikonyo alikuwa na ari ya kufanya biashara na alikuwa mfano bora kwa watu wengi katika sekta ya biashara kutokana na mafanikio yake.

Katika hotuba yake, naibu huyo wa Rais aliwataka viongozi kuiga mfano wa mzee Gikonyo kwa kukoma kuwadharau na kutowaheshimu wakenya, huku akiwahimiza kuwahudumia wananchi.

“Walio uongozini wanapaswa kuwaheshimu watu na kukoma kuwadharau. Wengine wanajigamba na mali waliyo nayo, huku wakisema serikali haina fedha na inakusanya ushuru kulipa madeni,” alisema Gachagua.

Mzee Gikonyo, ambaye alifariki wiki iliopita , alianza kufanya biashara mwaka wa 1930 akiwa mchuuzi jijini Nairobi.

Kwa muda wa miaka nyingi, alifanikiwa kupanua  biashara yake kwa jina Rwathia Group of Companies, ambayo ni kampuni inayomiliki  hoteli ya  Alfa, Magomano, Timboroa, New Kinangop, kampuni ya kusambaza mvinyo  ya Rwathia miongoni mwa mengine.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here