Home Habari Kuu Viongozi wa ODM Kilifi walumbana, wakazi wawasihi kutuliza joto la kisiasa

Viongozi wa ODM Kilifi walumbana, wakazi wawasihi kutuliza joto la kisiasa

0

Tofauti za kisiasa zimechacha miongoni mwa viongozi wa chama cha ODM katika kaunti ya Kilifi, hususan kati ya Gavana Gideon Mung’aro na Mwakilishi wa Wanawake Getrude Mbeyu. 

Mbeyu ameonyesha nia yya kuwania ugavana wa kaunti ya Kilifi mnamo mwaka wa 2027.

Siku chache zilizopita, wawakikishi wadi ambao ni wandani wa karibu wa Gavana Mung’aro walionekana kumshambulia hadharani Mbeyu kwa madai ya kuwa Mwakilishi huyo wa Wanawake amekuwa akimkosea heshima Mung’aro.

Huku tofauti kati ya viongozi wa ODM kaunti ya Kilifi zikitokota, wafuasi wa chama hicho eneo hilo wamewataka viongozi wa ODM kaunti ya Kilifi kukomesha malumbano yao ya mara kwa mara na badala yake washirikiane katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi.

Wakiongozwa na mwanaharakati wa kisiasa wa ODM kaunti ndogo ya Malindi Kensa Ondieki, wakazi hao wamewataka viongozi hao kukoma kumsuta Mbeyu na badala yake watekeleze majukumu yao.

Ni kauli ambayo imeungwa mkono na wengi wa wakazi wa Malindi akiwemo Emmanuel Okeyo pamoja na John Kitsao Luganje.

Wote hao wamewahimiza viongozi hao kuweka kando tofauti zao za kisiasa na badala yake washirikiane katika kutekeleza miradi ya maendeleo.

Wafuasi wa ODM hususan wamemsuta vikali Gavana Mung’aro kwa madai ya kuwatumia vibaraka wake kuwashambulia wapinzani wake.

Martin Mwanje & Dickson Wekesa
+ posts