Home Kimataifa Viongozi wa NATO wakutana nchini Lithuania

Viongozi wa NATO wakutana nchini Lithuania

0

Viongozi wa Umoja wa Kujihami wa Nchi za Kaskazini mwa Atlantiki, NATO leo Jumanne wanakusanyika katika mji mkuu wa Lithuania, Vilnius kushiriki mkutano wao wa kila mwaka. Licha ya tofauti zao, wanajaribu kuonyesha kuwa na umoja.

Watajadili kuongeza idadi ya nchi mpya wanachama kwenye umoja huo. Wanatazamia kuondoa baadhi ya mahitaji katika maombi ya Ukraine kujiunga na umoja huo lakini wametofautiana kuhusiana na maelezo mengine ya kina.

Jana Jumatatu, Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg alisema kuwa “Wajibu wa dharura zaidi kwa sasa ni kuhakikisha Ukraine inaendelea kuwa nchi huru na inayojitegemea barani Ulaya. Ikiwa Ukraine haitashinda, basi hakuna suala la uanachama la kujadiliwa kabisa.”

Maafisa katika Ikulu ya Urusi wanasema uanachama wa Ukraine unaweza ukawa tishio kwa Urusi. Msemaji wa ikulu hiyo Dmitry Peskov alisema hali kama hiyo itahitaji “mwitikio thabiti.”

Viongozi wa NATO tayari wanahaha kuhusiana na namna ya kuhakikisha raia wa Ukraine wanaweza kujilinda wenyewe.

Rais wa Marekani Joe Biden ameamua kukabiliana na upungufu wa makombora kwa kutuma mabomu ya kishada. Lakini washirika wake katika nchi za Uingereza, Canada na Uhispania wameonya juu ya hatari ya mabomu hayo kwa raia.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here