Home Habari Kuu Viongozi wa mashinani Siaya kuunga mkono serikali ya Kenya Kwanza

Viongozi wa mashinani Siaya kuunga mkono serikali ya Kenya Kwanza

0

Viongozi wa mashinani katika kaunti ya Siaya wamekubaliana kwa kauli moja kuunga mkono serikali ya Kenya Kwanza inayoongozwa na rais William Ruto.

Walikuwa wakizungumza kwenye mkutano katika makazi ya waziri wa teknolojia ya mawasiliano na uchumi digitali Eliud Owalo, huko Asembo leo.

Lengo la mkutano wa leo kulingana na Owalo lilikuwa kujadiliana kuhusu mipango ya maendeleo ambayo wangetaka kuona ikitekelezwa na namna ya kuitekeleza, na viongozi hao wapatao 350 kutoka wadi 30 waliorodhesha matatizo ambayo wangetaka yashughulikiwe na serikali kuu.

Changamoto hizo ni pamoja na ukosefu wa ajira kwa vijana, ukosefu wa maji safi ya kunywa, ukosefu wa stima mashinani, ukosefu wa usalama, huduma za matibabu, uzalishaji chakula na hali ya barabara zilizoharibiwa na mafuriko.

Waziri Owalo aliwahakikishia viongozi hao kwamba serikali ya kitaifa imejitolea kuhudumia wakenya katika pembe zote za nchi kwa usawa huku ikitekeleza ahadi zilizopo kwenye hati za maendeleo za kaunti.

Waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na mwenyekiti wa mamlaka ya maendeleo katika eneo la ziwa Dianga Waore, msemaji wa zamani wa polisi Charles Owino, Frederick Dor, Christopher Opondo na Collins Olemo.

Waziri Owalo ambaye pia alikutana na mbunge wa Gem Elisha Odhiambo, alisema kaunti ya Siaya ina uwezo mkubwa kimaendeleo na watu wanaohitajika wa kutumia fursa zilizopo.

Alisema kutokana na nia njema ya wakazi na uungwaji mkono kutoka kwa serikali anaona Siaya ikiinuka.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here