Home Habari Kuu Viongozi wa magharibi mwa Kenya walalamikia gharama ya juu ya maisha

Viongozi wa magharibi mwa Kenya walalamikia gharama ya juu ya maisha

0
Baadhi ya wabunge kutoka eneo la magharibi mwa nchi wameunyoshea utawala Kenya Kwanza kidole cha lawama kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha. 
Wakiongozwa na mbunge wa Bumula Jack Wamboka, viongozi hao waliozungumza wakati wa hafla moja iliyoandaliwa mjini Kakamega, walihusisha kupanda kwa gharama ya maisha na hatua ya utawala huo kuongeza ushuru mara kwa mara.
Wamboka alisema serikali ya sasa inapaswa kupunguza ushuru wa juu wanaotozwa Wakenya ambao umefanya maisha kuwa magumu mno.
Kauli zinazowadia wakati ambapo serikali imewataka Wakenya kukaza kamba ikisema ingawa ni kweli hali haitahimiliki kwa sasa, imeweka mikakati inayokusudia kuhakikisha Wakenya hawaelemewi na gharama ya juu ya maisha hivi karibuni.
Inasema baadhi ya mikakati hiyo ni utoaji wa mbei ya mbolea nafuu ya shilingi 2,500 na mbegu kwa wakulima katika hatua inayolenga kuhakikisha Kenya inajitosheleza kwa chakula.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, mbunge wa Likuyani aliwataka wakazi wa eneo bunge lake kutojihusisha na zoezi la usajili la chama UDA akidai chama hicho ni chanzo cha mateso yao.
Alidai eneo la magharibi mwa nchi ni ngome ya kisiasa ya kiongozi wa muungano wa Azimio Raila Odinga.
Kwa misingi hiyo, Gavana wa Kakamega Fernandes Barasa alitoa wito kwa wakazi kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha kama wanachama wa ODM wakati wa zoezi la usajili linaloendelea.