Baadhi ya wakazi wa kaunti ya Laikipia, wamemlaumu mbunge Mwangi kiunjuri wa Laikipia Mashariki na kiongozi wa wengi katika bunge la taifa Kimani Ichungwa ambao waliwaongoza wabunge 48 kumuidhinisha waziri wa usalama Prof. Kithure Kindiki kuwa kiongozi wa mlima Kenya.
Kulingana na wakazi hao, hatua hiyo ya wabunge hao, itazidisha migawanyiko katika eneo la mlima Kenya.
Wakazi hao wakiongozwa na naibu wa kitaifa wa chama cha Kiama kia Ma Njoroge Mugo, alionya kuwa hawatakubalia kutengwa kwa naibu wa Rais Rigathi Gachagua kupitia “Azimio la Nyahururu”.
Viongozi hao walisema hatua zozote zinapaswa kupitishwa kupitia ushiriki wa umma.
Mnamo siku ya Alhamisi wabunge 48, walisema ipo hapa ya kuwa na kiongozi ambaye atawaunganisha na uongozi wa serikali kuu kuhusu maswala ya maendeleo.
Wabunge hao walisema wanamuunga mkono waziri wa usalama wa taifa Prof. Kithure Kindiki.