Home Vipindi Viongozi wa Azimio washerehekea siku ya kuzaliwa ya Oburu Oginga

Viongozi wa Azimio washerehekea siku ya kuzaliwa ya Oburu Oginga

0
kra

Jumapili Oktoba 15, 2023, viongozi kadhaa wa muungano wa Azimio la Umoja One Kenya walikusanyika katika eneo la Bondo katika kaunti ya Siaya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Seneta wa kaunti hiyo Dkt. Oburu Oginga, kakake kiongozi wa muungano huo Raila Odinga.

Oburu ametimiza umri wa miaka 80 na katika ujumbe wa heri njema kwa kakake, Raila aliandika kuwa, “Oburu, kakangu mpendwa, ninakutakia siku njema ya kuzaliwa unapotimiza umri wa miaka 80! Tumepitia mengi pamoja na umesimama nami. Mungu azidi kukubariki.”

kra

Kiongozi mwenza wa muungano huo Kalonzo Musyoka ambaye alikuwa mgeni wa heshima wakati wa sherehe hiyo alimshukuru Oburu kwa mwaliko huku akimtakia mema. Alimsifia akisema ujasiri wake na kujitolea kwake kwa familia yake na pia kwa wananchi wa Kenya ni jambo la kupigiwa mfano.

Viongozi wengine waliokuwapo ni pamoja na Martha Karua, magavana James Orengo wa Siaya, Mutula Kilonzo Junior wa Makueni, Gladys Wanga wa Homa Bay, mkewe Raila, Mama Ida Odinga na wengine wengi.

Hafla hiyo ilijumuisha ibada na shughuli ya kukata keki.