Home Habari Kuu Viongozi wa Afrika Mashariki wakutana Arusha, wajadili mabadiliko ya tabia nchi

Viongozi wa Afrika Mashariki wakutana Arusha, wajadili mabadiliko ya tabia nchi

0

Marais wa Nchi na Wawakilishi wa Viongozi wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki walikutana Alhamisi jijini Arusha, Tanzania kwa Mkutano wa 23 kuhusu Mabadiliko ya Tabia  Nchi na Usalama wa Chakula.

Kikao hicho kilijadili njia za kutafuta majawabu dhidi ya athari za mabadiliko ya tabia nchi katika upatikanaji wa chakula yanayohusu moja kwa moja uhai wa nchi za Afrika Mashariki, watu, maendeleo na ustawi katika siku za usoni.

Rais William Ruto alisistiza kuwa uhifadhi wa mazingira ni swala nyeti Afrika Mashariki
na akaahidi kushikiniza kusainiwa kwa sheria zinazoshinikiza ukuaji mahususi wa mazingira wakati atakapohudhuria kongamano la kimataufa kuhusu mazingira la COP28.

Kikao hicho kiliongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania, na kuhudhuria na viongozi wengine wa serikali za ukanda wa Afrika Mashariki.

Website | + posts