Home Habari Kuu Vikao vya Seneti vyangóa nanga kaunti ya Turkana

Vikao vya Seneti vyangóa nanga kaunti ya Turkana

Vikao vya Bunge la Seneti vitaanza rasmi Jumatatu Adhuhuri mjini Lodwar katika kaunti ya Turkana na kuendelea hadi Ijumaa Septemba 29.

0

Vikao vya bunge la Seneti vilianza rasmi leo Jumatatu adhuhuri mjini Lodwar katika kaunti ya Turkana na vitaendelea hadi Ijumaa, Septemba 29.

Bunge hilo hufanya vikao vyake kwa awamu katika kaunti mbalimbali nchini kupitia kwa mpango wake wa Senate Mashinani.

Hii ni mara ya kwanza kwa vikao hivyo kuandaliwa katika kaunti ya Turkana.

Maseneta wengi waliwasili mjini Lodwar mapema leo Jumatatu wakiongozwa na Spika Amason Kingi.

Vikao vya bunge la Seneti katika kaunti ya Turkana vitapeperushwa na runinga ya taifa ya KBC Channel 1, Radio Taifa na Idhaa ya Kiturkana.