Home Habari Kuu Vijana wahimizwa kukumbatia taasisi za kiufundi

Vijana wahimizwa kukumbatia taasisi za kiufundi

Kulingana na Dorcas enzi ambapo watu walienda shule ili wapate ajira za afisini zimeisha.

0
Mke wa Naibu Rais Mchugaji Dorcas Rigathi.

Mke wa naibu Rais Mchungaji Dorcas Rigathi, ametoa wito kwa vijana hapa nchini kukumbatia taasisi za kutoa mafunzo ya kiufundi.

Akizungumza katika taasisi ya kiufundi ya Giathugu iliyoko eneo la Mukurweini kaunti ya Nyeri wakati wa uzinduzi wa mpango wa 2JIAJIRI, Dorcas alisema wakati umewadia kwa taifa hili kubadili jinsi ya kutekeleza mambo na kuwahimiza vijana ambao hawakupata fursa ya kujiunga na vyuo vikuu, kujiunga na taasisi za mafunzo ya kiufundi.

“Taasisi za kiufundi zinatekeleza wajibu wa kuwaandaa vijana kuwa na uwezo wa kujiimarisha kiuchumi na kuwa watu wa kujitegemea,” alisema Dorcas.

Kulingana na Dorcas enzi ambapo watu walienda shule ili wapate ajira za afisini zimeisha.

“Tunapaswa kubadili jinsi ya kutekeleza mambo,”alisisitiza Mchungaji Dorcas.

Matamshi yake yaliungwa mkono na naibu Gavana wa Nyeri David Kinanire na mbunge wa Mukurweini John Kaguchia.