Home Kaunti Vijana wa ODM kaunti ya Nairobi wawafokea MCAs wake kwa...

Vijana wa ODM kaunti ya Nairobi wawafokea MCAs wake kwa usaliti na kufanya kazi na gavana Sakaja

0

Vijana wa chama cha ODM kaunti ya Nairobi wamewafokea waakilishi wadi wa chama hicho kwa usaliti na kufanya kazi na serikali ya Gavana Johnson Sakaja .

Kwenya kikao na Wanahabari siku ya Jumamosi waliataja hatua hiyo ya waakilishi bunge la kaunti kuwa unafiki na usaliti, wakiongeza kuwa wametelekeza majukumu yao walivyochaguliwa na wapiga kura.

Vijana hao pia walimshutumu Gavana Sakaja kwa utepetevu na kukosa kuwajibika huku wakielekeza lawama kwa MCA hao wa ODM, wanaostahili kumkosoa Gavana lakini badala yake wanamuunga mkono.

Walitaja baadhi ya changamoto katika kaungi ya nairobi kama vile uzoaji wa taka,kutpakaa kwa maji taka,upungufu wa maji lichja mvua kubwa inayonyesha na ujenzi mbovu .

Vijana hao wamewataka waakilishi wodi hao kujirejelea na kutekeleza wajibu wao waliopewa na wapiga kura .