Home Habari Kuu Vijana ni nguzo muhimu kwa maendeleo ya Afrika, asema Gachagua

Vijana ni nguzo muhimu kwa maendeleo ya Afrika, asema Gachagua

Waziri Emma, ambaye ana umri wa miaka 28, ni miongoni mwa waziri wachanga zaidi barani Afrika.

0
Naibu rais Rigathi Gachagua na waziri wa habari, Mawasiliano na teknolojia wa Namibia Emma Inamutila Theofelus.

Naibu Rais Rigathi Gachagua, amesema uongozi wa vijana ni nguzo muhimu katika maendeleo ya bara Afrika, akidokeza kuwa vijana wanatekeleza wajibu muhimu kulinda siku za baadaye za bara hili.

Akizungumza Jumatano alipokuwa mwenyeji wa waziri wa habari, mawasiliano na teknolojia wa Namibia Emma Inamutila Theofelus katika makazi yake mtaani Karen, naibu huyo wa Rais alisema anatambua jukumu linalotekelezwa na vijana katika kuchangia maendeleo ya bara hilo.

Waziri Emma, ambaye ana umri wa miaka 28, ni miongoni mwa waziri wachanga zaidi barani Afrika.

Gachagua alimpongeza waziri huyo kwa kupanda ngazi hadi kwa wadhifa huo akiwa na umri mdogo, akisema yeye ni kielelezo kwa kizazi chake.

“Kuwa waziri na umri wa miaka 28 ni ufanisi mkubwa, ninatazamia hayo kufanyika katika nchi yetu,” alisema Gachagua.

Waziri huyo, yuko hapa nchini kwa mkutano wa  Connected Africa 2024, unaoandaliwa katika bustani ya Uhuru Jijini Nairobi.

Kwa upande wake, waziri Emma alimshukuru naibu wa Rais kwa kuchukua wajibu wa kuwakuza vijana.

“Tunakushukuru kwa kuchukua nafasi muhimu ya  kuwakuza vijana,” alisema waziri Emma.

Waziri huyo aliipongeza Kenya kwa kupiga hatua kubwa katika maswala ya teknolojia barani Afrika.

Website | + posts