Home Kimataifa Vijana kunufaika na ujuzi wa kidijitali Magharibi mwa nchi

Vijana kunufaika na ujuzi wa kidijitali Magharibi mwa nchi

kra

Maelfu ya vijana katika kaunti za Bungoma na Kakamega wanatarajiwa kunufaika na mafunzo ya ujuzi wa kidijitali ili waweze kuajiriwa katika mitandao ya kidijitali.

Mafunzo hayo yatatolewa kwa ushirikiano baina ya Julius Mwale, mwekezaji mkuu katika kituo cha matibabu na teknolojia cha Mwale, wakfu wa DRM na kampuni ya masuala ya teknolojia ya INUA AI.

kra

Mwale alisema vijana watanufaika kutokana na mafunzo kuhusu akili unde, ushauri na mipango ya mafunzo kazini ambazo zitawawezesha kuajiriwa.

Huku ripoti za hivi punde zikionesha kuwa eneo la Webuye kaunti ya Bungoma, lina zaidi ya wasichana wajawazito 26,000 na wengine 1,600 walio na virusi vya ukimwi wenye umri kati ya miaka  10 na 24 kufikia mwezi Juni mwaka 2023, mafunzo hayo yanalenga kuwawezesha vijana kujipatia riziki.

Tangazo hilo la ushirikiano lilitolewa wakati wa uzinduzi wa michezo ya wakfu wa D-RM ya Aprili katika uwanja wa Sitikho huko Webuye. Michezo hiyo inalenga kukuza mitindo bora ya maisha.