Home Kaunti Vijana kaunti ya Kwale wahimizwa kuwa mabalozi wa amani

Vijana kaunti ya Kwale wahimizwa kuwa mabalozi wa amani

Achani aliwahimiza vijana kutotumiwa na wanasiasa walio na ubinafsi, wanaochukua fursa ya hali ilivyo nchini kusambaratisha uthabiti wa taifa hili.

0
Gavana wa Kwale Fatuma Achani.
kra

Gavana wa kaunti ya Kwale Fatuma Achani, ametoa wito kwa vijana katika eneo la Diani kaunti ndogo ya  Msambweni, kudumisha sheria na kuwa mabalozi wa amani, ikizingatiwa eneo hilo ni kivutio cha watalii.

Matamshi ya Gavana huyo yanajiri baada ya maandamano kushuhudiwa kote nchini kupinga Mswada wa fedha 2024, yaliyosababisha maafa na uharibifu wa mali.

kra

Achani aliwaonya vijana dhidi ya kusababisha vurumai na kuvuruga amani katika eneo la Diani, akisema hatua hiyo itaathiri uchumi wa eneo hilo ambalo hutegemea pakubwa sekta ya utalii.

“Tumpe Rais muda wa kushughulikia maswala yaliyoibuliwa, hasaa ikitiliwa maanani hakuidhinisha mswada huo wa fedha,” alisema Achani.

Aidha Achani aliwahimiza vijana kutotumiwa na wanasiasa walio na ubinafsi, wanaochukua fursa ya hali ilivyo nchini kusambaratisha uthabiti wa taifa hili.

“Taifa hili haliwezi kujengwa kupitia ghasia, tukumbatie mazungumzo kwani hiyo ndio njia pekee ya kupeleka taifa hili mbele,’ alisema Gavana huyo.

Alitoa wito kwa maafisa wa polisi kuwatia nguvuni wahalifu wanaowahangaisha wakazi wa eneo hilo, huku akiwataka wananchi kutoa habari kwa asasi za usalama kuhusu wanaotekeleza uhalifu katika eneo hilo la Diani.

Website | + posts