Home Biashara Vijana 1,500 kuajiriwa katika eneo maalum la kiuchumi Naivasha

Vijana 1,500 kuajiriwa katika eneo maalum la kiuchumi Naivasha

Katibu katika wizara ya biashara  na viwanda Abubakar Hassan Abubakar, alisema kiwanda cha kutengeneza magari cha Tad Motors, kitaanza shughuli zake katika eneo maalum la kiuchumi la Naivasha katika muda wa miezi sita ijayo.

0
Katibu katika wizara ya biashara na viwanda Abubakar Hassan Abubakar, azuru eneo la kiuchumi la Naivasha.
kra

Vijana 1,500 huenda watanufaika pakubwa katika eneo maalum la kiuchumi la Naivasha, huku serikali ikilenga kubuni nafasi za ajira katika kiwanda cha utengenezaji wa magari yanayotumia nguvu za umeme.

Katibu katika wizara ya biashara  na viwanda Abubakar Hassan Abubakar, alisema kiwanda cha kutengeneza magari cha Tad Motors, kitaanza shughuli zake katika eneo maalum la kiuchumi la Naivasha katika muda wa miezi sita ijayo.

kra

Akizungumza wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda cha kampuni hiyo, katibu huyo, alisema serikali itatumia maeneo  maalum ya kiuchumi nchini kuzindua nafasi za kazi kwa mamia ya vijana nchini.

“Uwekezaji huu utabuni nafasi 100 za ajira wakati wa ujenzi wa kiwanda hiki, na nafasi 1,500 wakati kitakapoanza shughuli zake katika muda wa miezi sita ijayo,” alisema Abubakar.

Kampuni hiyo ya Tad Motors, imewekeza dola milioni tatu kwenye eneo hilo la kiuchumi, kujenga kiwanda cha magari hayo yanayotumia nguvu za umeme, yatakayouzwa humu nchini na katika soko la kimataifa.