Home Kimataifa Vidosho wa Kenya kuwinda dhahabu telezi ya mita 10,000 Olimpiki

Vidosho wa Kenya kuwinda dhahabu telezi ya mita 10,000 Olimpiki

0
kra

Bingwa wa Olimpiki katika mita 5,000 Beatrice Chebet atawaongoza Margaret Chelimo na Lillian Kasait huku Kenya ikiwinda dhahabu ya kwanza ya mita 10,000 Ijumaa usiku jijini Paris, Ufaransa.

Fainali hiyo itaanza dakika 3 kabla ya saa nne usiku, huku Kenya ikisaka dhahabu ya pili kwenye makala ya mwaka huu ya Olimpiki.

kra

Hata hivyo, upinzani kwa Wakenya unatarajiwa kutoka kwa bingwa mtetezi Sifan Hassan wa Uholanzi na Wahabeshi Tsigie Gebreselama, Fortyen Tesfaye na Gudaf Tsegay.

Kenya imenyakua nishani mbili za fedha katika historia ya Olimpiki kupitia kwa Sally Kipyego mwaka 2012 na Vivian Cheruiyot mwaka 2016.

Website | + posts