Home Michezo Victorien Adebayor kuchezea Simba SC ya Tanzania

Victorien Adebayor kuchezea Simba SC ya Tanzania

0

Mchezaji wa mpira wa miguu Victorien Adebayor huenda akachezea klabu cha Simba SC kwenye ligi kuu nchini Tanzania. Wing’a huyo alionekana jijini Dar es Salaam Jumamosi ambapo alishiriki mazungumzo na wasimamizi wa Simba kwa takriban dakika 40.

Katika kikao hicho, Adebayor mzaliwa wa Niger alishawishiwa kujiunga na Simba SC, na inasemekana kwamba alikubali kujiunga na ligi kuu ya Tanzania. Mchezaji huyo wa timu ya RS Berkane ya Morocco yuko tayari kutia saini mkataba wa miaka miwili na timu hiyo ya Tanzania ukiwepo uwezekano wa kuongeza kandarasi yake kwa muda wa mwaka mmoja.

Kilichosalia sasa ni Simba SC kuanza mashauriano na RS Berkane kuhusu kumsajili Adebayor ambaye anataka kupatiwa nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha Simba SC baada ya kutochezeshwa kwa muda na RS Berkane.

Victorien Adebayor au ukipenda Adebayor Zakari Adje ana umri wa miaka 26 na huenda akajiunga na wachezaji wengine wa Simba SC kwenye Kambi mwezi ujao kujiandaa na msimu mpya wa mwaka 2023-2024.

Website | + posts