Home Kimataifa Venezuela yarejeshewa vikwazo na Marekani

Venezuela yarejeshewa vikwazo na Marekani

0

Marekani imeanza kurejesha baadhi ya vikwazo ambavyo ilikuwa imewekea taifa la Venezuela awali kwa kubana sekta yake ya uchimbaji madini.

Haya yanafuatia hatua ya makahama ya upeo ya Venezuela ya kudumisha kupigwa marufuku kwa mwaniaji urais wa upinzani kutoka kwenye siasa kwa muda wa miaka 15.

Kampuni zote za Marekani ambazo zinafanya biashara na kampuni ya serikali ya Venezuela ya uchimbaji madini Minerven zimepatiwa muda hadi Februari 13, 2024 kufunga biashara zinazoendelea.

Marekani ilitoa onyo kwa Venezuela mwishoni mwa juma kwamba ingerejesha vikwazo vilivyolegezwa mwaka jana iwapo haingetekeleza mapatano yao.

Mwaka jana, Marekani ilikubali kuondoa baadhi ya vikwazo huku Venezuela ikitakiwa pia kulegeza kamba kwa wanasiasa wa upinzani waliopigwa marufuku kuanzisha mchakato wa kupinga marufuku dhidi yao.

Ijumaa mahakama hiyo ya upeo ambayo inapendelea serikali ya Rais Nicolas Maduro ilidumisha marufuku ya miaka 15 dhidi ya kiongozi wa upinzani Maria Corina Machado.

Mahakama hiyo pia ilikatalia mbali pendekezo la mahali pa Machado kuchukuliwa na Henrique Capriles kwa kile ilichokitaja kuwa hastahiki kuwania Urais.

Machado ametaja hatua ya mahakama ya kumbania asiwanie Urais kuwa uhalifu wa mahakama na kuapa kusalia kwenye kinyang’anyiro.

Kulingana na Machado uamuzi wa mahakama ya upeo ni dhihirisho kwamba chama tawala kinaogopa kupambana naye kwenye uchaguzi.

Website | + posts