Home Habari Kuu Vanessa Ogema aachiliwa kwa dhamana ya laki mbili

Vanessa Ogema aachiliwa kwa dhamana ya laki mbili

0

Mwanamke aliyerekodiwa kwenye video akidaiwa kuwadhulumu na kuwarushia wahudumu wa afya cheche za maneno katika hospitali ya Port Victoria, kaunti ya Busia ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi 200,000. 

Vanessa Ogema alifikishwa mahakamani akikambiliwa na mashtaka manne.

Mashtaka yaliyowasilishwa dhidi yake ni pamoja na kuwadhulumu wahudumu wa afya hospitalini hapo na kutatiza utoaji bora wa huduma za afya kwa wagonjwa.

Ogema mwenye umri wa miaka 23 alikanusha mashtaka yote dhidi yake.

Waziri Susan Nakhumicha na vyama vya wahudumu wa afya vililaani kitendo cha mwanafunzi huyo wa chuo cha wanawake cha hospitali ya Nairobi Womens na kutaka hatua kali kuchukuliwa dhidi yake.

Kumekuwa na lalama kuwa visa vya dhuluma dhidi ya wahudumu wa afya vinaongezeka nchini huku wadau wakitaka hali hiyo kuangaziwa.

Website | + posts