Home Burudani Vanesa Chettle kusaidiwa na Gavana Bii

Vanesa Chettle kusaidiwa na Gavana Bii

0
kra

Mwanamitandao Vanesa Cheruto maarufu kama Vanesa Chettle hatimaye amekutana na Gavana wa kaunti ya Uasin Gishu Jonathan Bii ambaye ameanza shughuli ya kumsaidia kurejelea maisha ya kawaida.

Oga Obinna alichapisha video akiwa kwenye mkutano na Gavana Bii, Cheruto, Dem wa Facebook na wengine ambapo Bii alisema kwamba yeye na wanawe kupitia wakfu wao wa Chelilim wameamua kumsaidia.

kra

Awali katika mahojiano Obinna alimfahamisha Gavana Bii kuhusu kisa cha Vanessa ambaye alisema anahitaji kusaidiwa kujikimu kimaisha.

Vanessa aliomba Gavana kitu ambacho kinaweza kumsaidia kama vile biashara ambapo alitaja biashara ya kilimo ikitizamiwa kwamba kaunti ya Uasin Gishu ni eneo la kilimo.

Kuhusu kupelekwa katika kituo cha kurekebisha tabia, Vanessa ambaye alikiri kwamba anatumia dawa za kulevya alichagua kupata ushauri nasaha badala ya kituo hicho.

“Naonelea nipate ushauri nasaha kwa sababu kuniachisha dawa za kulevya mara moja hakutasaidia. Kuna sababu inayosababisha nitumie dawa hizo za kulevya. Sababu hiyo inaweza kutatuliwa kupitia ushauri nasaha.” alisema Vanessa.

Chettle aliwahi kuhusika kwenye kipindi cha matukio halisi Nairobi Diaries na alifahamika na wengi kupitia mitandao. Anasema aliolewa akiwa na umri wa miaka 18 pekee na mume wake alikuwa wa umri wa zaidi ya miaka 60.

Anadai kwamba alitengwa na familia yake kwa sababu hiyo,  ndoa hiyo ilisambaratika na hana namna ya kujikimu.

Website | + posts