Home Michezo Van der Sar ahamishiwa hospitali ya nyumbani kutoka Croatia

Van der Sar ahamishiwa hospitali ya nyumbani kutoka Croatia

Van der Sar atasalia katika chumba cha wagonjwa mahututi kulingana na mkewe.

0

Mlinda lango wa zamani wa Uholanzi Edwin Van Der Sar,amehamishwa kutoka hospitali moja nchini Croatia hadi ile ya nyumbani Uholanzi kupokea matibabu kutoka na kuvuja kwa damu kwenye ubongo.

Van der Sar atasalia katika chumba cha wagonjwa mahututi kulingana na mkewe.

Kipa huyo wa zamani wa Manchester United aliye na umri wa miaka 52, alikuwa likizoni nchini Croatia alipougua na kulazwa hospitalini wiki moja iliyopita.

Van Der Sar alistaafu kutoka soka mwaka 2011 na aliichezea Man U mechi 266 na kushinda mataji manne ya ligi kuu Uingereza na kombe la ligi ya mabingwa mwaka 2008.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here