Home Kimataifa Uzinduzi wa kitambulisho cha kidijitali umeahirishwa

Uzinduzi wa kitambulisho cha kidijitali umeahirishwa

Rais William Ruto, alitarajiwa kuongoza uzinduzi huo tarehe mbili mwezi Oktoba katika kaunti ya Nakuru.

0
Katibu katika idara ya uhamiaji, Julius Bitok.

Uzinduzi wa Maisha Namba na kitambulisho cha kidijitali uliokuwa uandaliwe siku ya Jumatatu ijayo, umeahirishwa, hayo ni kulingana na katibu katika idara ya uhamiaji na huduma kwa wananchi Julius Bitok.

Kupitia kwa taarifa, Bitok alisema tarehe mpya ya uzinduzi huo itatangazwa hivi karibuni.

Rais William Ruto, alitarajiwa kuongoza uzinduzi huo tarehe mbili mwezi Oktoba katika kaunti ya Nakuru.

Hata hivyo Bitok alisema kwamba shughuli ya kupokea maoni kutoka kwa umma na wadau wengine kuhusu Maisha Namba na kitambulisho cha kidijitali, itaendela kama ilivyopangwa.

Bitok awali alisema kwamba kitambulisho cha kidijitali kitakuwa cha lazima kwa wanaotuma maombi kwa mara ya kwanza na kwa wale wanaochukua vitambulisho vipya kutokana na vyao kupotea.

Bitok alisema kwamba kutakuwa na mfumo kuu wa takwimu uitwao sajili kuu ya kitaifa ya idadi ya watu yenye taarifa zote za kitambulisho cha kila Mkenya.

Kulingana na katibu huyo, Maisha Namba, itakuwa kitambulisho cha kizazi cha tatu na kuchukua nafasi ya kitambulisho cha kizazi cha pili. Kitambulisho hicho kitaimarishwa na kukifanya vigumu kukighushi.

Website | + posts