Home Biashara Uzalishaji wa matunda Uganda: Museveni alenga soko la kimataifa

Uzalishaji wa matunda Uganda: Museveni alenga soko la kimataifa

0

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameilimbikizia sifa kampuni ya Harris International kutokana na kile alichokitaja kuwa mchango mkubwa uliofanywa na kampuni hiyo katika kukuza ukuaji uchumi wa nchi hiyo. 

Akizungumza alipokutana na mwenyekiti wa kampuni hiyo Yasser Ahmed, Museveni alisema kampuni ya Harris International imekuwa mstari wa mbele katika kuunganisha uzalishaji wa matunda na soko la ndani la nchi hiyo.

 Anasema sasa anataka uzalishaji wa matunda wa nchi hiyo kuunganishwa na soko la nje.

“Sisi ni nchi thabiti zaidi katika kilimo, kila kitu kinakua hapa tumekuwa tukipanda bidhaa tangu kitambo. Kwa hivyo, watu kama Yasser walipokuja, tulikuwa tayari tunahamasisha upanzi wa matunda kwa ajili ya biashara. Tuliwataka watu kuanza kupanda matunda katika maeneo kama vile Soroti, Luwero, Kayunga na Masaka,” alisema Rais Museveni baada ya mkutano kati yao.

Aliongeza kuwa ukosefu wa uchakataji ulirudisha nyuma kilimo hicho, hali ambayo imesuluhishwa kutokana na ujio wa kampuni ya Harris International.

Website | + posts