Home Biashara Uzalishaji mahindi Kenya umepungua kwa magunia milioni 10

Uzalishaji mahindi Kenya umepungua kwa magunia milioni 10

0

Uzalishaji wa mahindi humu nchini umepungua kwa magunia milioni 10.9 katika kipindi cha miaka mitano hadi mwezi Disemba mwaka 2022, hatua ambayo ni pigo kwa juhudi za nchi kuhakikisha usalama wa chakula.  

Data kutoka kwa Idara ya Taifa ya Takwimu Nchini, KNBS zinaashiria kuwa uzalishaji wa mahindi ulipungua kutoka magunia 44.6 yaliyovunwa mwaka 2018 hadi milioni 34.3 mwaka jana, upungufu ambao ni mkubwa zaidi katika kipindi cha mwongo mmoja.

Licha ya juhudi za serikali kuwasaidia wakulima kupitia utoaji ruzuku kwa mbegu na mbolea, uzalishaji wa mahindi umeendelea kupungua kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita mfululizo.

“Uzalishaji wa mahindi ulipungua kwa asilimia 6.5 kutoka magunia milioni 36.7 mwaka 2021 hadi magunia milioni 34.3 mwaka 2022, kwa kiwango kikubwa kutokana na hali mbaya ya hewa mnamo mwaka wa 2022,” ilielezea KNBS.

Uzalishaji wa mahindi nchini ulipungua hadi kufikia magunia milioni 44 mwaka wa 2019, magunia milioni 42.1 mwaka 2020 na magunia milioni 36.7 mwaka 2021 kulingana na Ripoti ya Utafiti wa Kiuchumi ya KNBS ya Mwaka 2023.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here