Home Taifa Uvuvi utachochea ukuaji wa nchi kiuchumi, asema Rais Ruto

Uvuvi utachochea ukuaji wa nchi kiuchumi, asema Rais Ruto

0
kra

Rais William Ruto ametaja sekta ya uvuvi kuwa muhimu zaidi katika kuchochea ukuaji wa nchi hii kiuchumi. 

Aidha, ameitaja sekta hiyo kuwa kiungo muhimu kwa ajenda ya serikali ya Kenya Kwanza ya mabadiliko ya kiuchumi kuanzia chini hadi juu.

kra

Kulingana na Ruto, ikiwa itafanyiwa uwekezaji mzuri, sekta ya uvuvi inaweza ikaileta nchi hii mabilioni ya fedha kusaidia kuhuisha uchumi wake.

“Hiyo ndio sababu tunawekeza katika uchumi wetu wa samawati ili kufungua uwezo wake mkubwa. Mpango huu wa makusudi utaleta mapato ya shilingi bilioni 120 kwa mwaka na kubuni nafasi za ajira kwa maelfu ya vijana,” alisema Rais Ruto leo Ijumaa wakati wa ziara yake katika eneo la Pwani.

Aliandamana na Magavana Abdulsalam Shariff Nasir (Mombasa) Fatuma Achani (Kwale), Issa Timamy (Lamu), Godhana Dhadho (Tana River), wabunge na wawakilishi wadi.

Wakati wa ziara hiyo, Rais Ruto alitoa ruzuku ya shilingi bilioni 1.7 kwa makundi 612 ya uvuvi kutoka kaunti za Mombasa, Tana River, Kwale, Lamu na Kilifi.