Home Vipindi Utoaji zabuni Machakos: Idara zote zatakiwa kuwapatia vijana fursa

Utoaji zabuni Machakos: Idara zote zatakiwa kuwapatia vijana fursa

0
kra

Gavana wa kaunti ya Machakos Wavinya Ndeti amezielekeza idara zote za kaunti hiyo kuhakikisha vijana wanapatiwa fursa za kapata zabuni za serikali. 

Wavinya amesema serikali yake imejitolea kutii kifungu cha 55 cha katiba kinachohitaji vijana kuhusika katika ujenzi wa taifa.

kra

“Nimezielekeza idara zote kutenga zabuni kwa ajili ya vijana,” alitangaza Wavinya wakati wa makongamano ya ushiriki wa umma kwa marekebisho yaliyopendekezwa kwa Sheria ya Uwezeshaji Vijana 2024 katika kaunti ya Machakos.

Makongamano hayo yalifanyika katika kaunti ndogo za Mavoko na Machakos.