Home Kimataifa Uteuzi wa Soi kama Waziri wa Jinsia wakataliwa na bunge

Uteuzi wa Soi kama Waziri wa Jinsia wakataliwa na bunge

0
kra

Kamati ya Bunge la Taifa kuhusu uteuzi imekataa uteuzi wa Stella Soi Langat kama Waziri wa Jinsia, Utamaduni, Sanaa na Urithi.

Wengine 19 walioteuliwa mawaziri na Rais William Ruto wameidhinishwa na kamati hiyo baada ya usaili uliodumu siku tatu.

kra

Usaili hao ulianza Agosti 1-4, 2024.

Baada ya kuapishwa, Opiyo Wandayi atakuwa Waziri wa Kawi, John Mbadi awe Waziri wa fedha, Kipchumba Murkomen Waziri wa Michezo, Salim Mvurya Waziri wa Biashara, Rebecca Miano Waziri wa Utalii huku Alfred Mutua akihudumu kama Waziri wa Leba.

Wengine ni pamoja na Ali Hassan Joho Waziri wa Madini na Uchumi Samawati, Wycliffe Oparanya Waziri wa Vyama vya Ushirika na Justin Muturi Waziri waUutumishi wa Umma.

Suala la uteuzi wa Soi sasa litajadiliwa na bunge lote ambalo huenda likabatilisha uamuzi wa kamati kuhusu uteuzi huo au likashikilia msimamo sawa.

Kisa hiki ni cha pili kushuhudiwa chini ya serikali ya Kenya Kwanza ambapo uteuzi wa Penina Malonza kama Waziri ulikataliwa na kamati lakini bunge likauidhinisha na alihudumu katika Baraza lililovunjwa la Mawaziri.

Website | + posts