Home Kimataifa Utawala wa jeshi nchini Burkina Faso waongezwa kwa miaka mitano

Utawala wa jeshi nchini Burkina Faso waongezwa kwa miaka mitano

0

Serikali ya kijeshi nchini Burkina Faso umejiongezea muda wa kutawala kwa kipindi cha miaka mitano zaidi huku kiongozi wa kijeshi Ibrahim Traoré, akiruhusiwa kugombea kiti cha Urais baada ya kipindi hicho.

Traore aliahidi kurejesha hali ya kawaida alipotwaa mamlaka takriban miaka miwili iliyopita pamoja na kurejesha serikali ya raia kuanzia Julai mosi mwaka huu.

Hatua ya hivi punde inashuhudia Burkina Faso ikijiunga na Mali ambao pia waliongeza kipindi cha utawala wa jeshi.

Burkina Faso imekuwa chini ya utawala kijeshi tangu Jnuari mwaka 2022, wakati Kanali Paul-Henri Damiba alitwaa mamlaka kutoka kwa aliyekuwa Rais Roch Kaboré.