Home Kaunti Uswidi kupiga jeki miradi ya maendeleo kaunti ya Makueni

Uswidi kupiga jeki miradi ya maendeleo kaunti ya Makueni

0
Balozi wa Uswidi hapa nchini Caroline Vicini (Kushoto), na Gavana wa Makueni Mutula Kilonzo Jnr.
kra

Serikali ya Uswidi inalenga kushirikiana na serikali ya kaunti ya Makueni kupiga jeki maendeleo katika kaunti hiyo.

Hata hivyo, Balozi wa Uswidi hapa nchini Caroline Vicini amesema ushirikiano huo utategemea uwazi na uwajibikaji wa jinsi fedha zinatumiwa katika kaunti hiyo.

kra

“Serikali ya kaunti ya Makueni inapaswa kuwajibikia matumizi ya fedha. Uwazi na uwajibikaji ni muhimu sana kwetu,” alisema Vicini baada ya kukutana na Gavana wa Makueni Mutula Kilonzo Jr siku ya Jumatatu.

Balozi huyo alisema serikali yake inalenga kushirikiana na kaunti ya Makueni katika maswala ya mabadiliko ya tabia nchi, mazingira na maji, ambayo ni changamoto kuu katika eneo hilo.

“Makueni inakabiliwa na changamoto kuu ya maji, na tumetilia maanani swala hilo. Tutahusika na kusaidia kwa njia moja au nyingine,” alisema Balozi huyo.

Kwa upande wake, Gavana Mutula Kilonzo Jr alisema serikali ya Uswidi imekubali kushirikiana na kaunti ya Makueni kwa misingi kwamba ushirikiano huo utakuwa wazi na wenye uwajibikaji.

“Balozi amekubali kushirikiana na Makueni, bila kuwepo kwa visa vyovyote vya ufisadi,” alisema Gavana Mutula.

Website | + posts