Home Kimataifa Usimteme Aisha Jumwa, viongozi wa Kilifi wamsihi Ruto

Usimteme Aisha Jumwa, viongozi wa Kilifi wamsihi Ruto

0
kra

Viongozi wa kaunti ya Kilifi wametoa wito kwa Rais William Ruto kuhakikisha hamwachi nje Aisha Jumwa wakati anapoedelea kuunda upya serikali yake. 

Jumwa, ambaye ni mwandani wa Rais Ruto, alihudumu kama Waziri wa Jinsia katika Baraza la Mawaziri lililovunjwa, wadhifa ambao tayari ameupoteza.

kra

Hii ni baada ya kuteuliwa kwa Stella Soi Lang’at kuhudumu katika wadhifa huo, uteuzi ambao sasa unasubiri tu idhini ya bunge.

Hata hivyo, wakizungumza katika kaunti ya Kilifi, viongozi hao wakiongozwa na Gavana wa Kilifi Gideon Mung’aro, walitoa wito kwa Rais Ruto kuhakikisha Jumwa yuko serikalini.

Walielezea kuwa litakuwa jambo la kusikitisha ikiwa Jumwa ataachwa nje ya serikali ikizingatiwa alihudumu kama Waziri.

Jumwa ameelezea imani kwamba ataendelea kuhudumu serikalini.

Akizungumza mjini Watamu, kaunti ya Kilifi wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa soko la kisasa litakaloghirimu shilingi milio 20, Rais Ruto amewahakikishia viongozi na wakazi wa Kilifi anakotoka Jumwa kwamba Jumwa ataendelea kuhudumu katika serikali yake.

Hata hivyo, haijabinika ni wadhifa gani ambao Jumwa atakabidhiwa ikizingatiwa umesalia wadhifa mmoja tu wa uwaziri ambao umesalia baada ya kuteuliwa kwa mawaziri 20, ukiwa ni ule wa Waziri wa Jumuiya ya Afrika.

Wadhifa huo awali ulishikiliwa na Peninah Malonza.

 

 

Jumwa ali

Martin Mwanje & Dickson Wekesa
+ posts