Home Habari Kuu Usalama waimarishwa Nairobi wakati Kongamano la Tabia Nchi liking’oa nanga

Usalama waimarishwa Nairobi wakati Kongamano la Tabia Nchi liking’oa nanga

0

Maelfu ya maafisa wa usalama wameshika doria kila pembe ya jiji kuu la Kenya, Nairobi wakati Kongamano la Afrika kuhusu Tabia Nchi likianza jijini humo leo Jumatatu. 

Serikali inasema maafisa wapatao 4,000 watakuwa macho kuhakikisha usalama unadumishwa wakati wa kongamano hilo la siku tatu.

Wajumbe wapatao 30,000 wanatarajiwa kuhudhuria kongamano hilo litakaloandaliwa katika jumba la mikutano ya kimataifa la Kenyatta, KICC.

Rais William Ruto anatarajiwa kufungua rasmi kongamano hilo leo Jumatatu.

“Idara ya Usalama wa Taifa imeweka mipango kabambe ya usalama ili kuhakikisha usalama wa wajumbe watakaohudhuria kongamano hilo punde baada ya kuwasili, wakati wakiishi na watakapoondoka nchini baada ya kongamano hilo,” amesema Katibu katika Wizara ya Usalama wa Taifa Dkt. Raymond Omollo.

Dkt. Omollo aidha anasema serikali imeandaa mpango madhubuti wa kuitikia hali za dharura zisizotazamiwa haraka iwezekanavyo.

 

 

 

Website | + posts