Home Kimataifa Urusi yatuma tani laki mbili za nafaka Afrika

Urusi yatuma tani laki mbili za nafaka Afrika

0

Urusi imetangaza kutuma shehena ya kwanza ya nafaka kwa mataifa ya Afrika kutimiza ahadi ya rais Vladmir Putin, wakati wa kongamano la mataifa ya Afrika mwezi Julai mwaka huu.

Kulingana na waziri wa kilimo wa Urusi Dimitry Patrishev, shehena hiyo iliondoka Urusi Ijumaa ikibeba tani laki mbili zitakazosafirishwa kwa mataifa sita ya Afrika.

Shehena ya kwanza itasafirishwa hadi nchini Burkina Fasso na Somalia huku shehena nyingine zikitarajiwa kutumwa Zimbabwe,Mali,Jamhuri ya Afrika ya kati na Eritrea.

Website | + posts