Wajumbe wanaohudhuria mkutano wa maandalizi ya Mkutano wa Mapitio wa Mwaka 2026 wa Mkataba wa Kuzuia Ueneaji wa Silaha za Nyuklia, NPT unaofanyika nchini Austria walimsikiliza mwakilishi wa Urusi Mikhail Kondratenkov jana Jumanne.
Kondratenkov alisema Umoja wa Kujihami wa Nchi za Kaskazini mwa Atlantiki, NATO umekuwa “kambi ya kijeshi ya kinyuklia” ambayo uwezo wake wa kimkakati kwa pamoja unazidi ule wa Urusi.
Mwakilishi wa Poland Adam Bugajski aliwakosoa Warusi kwa kupeleka silaha za nyuklia nchini Belarus akiitaja hatua hiyo kuwa inayokiuka ahadi zao chini ya NPT.
Kadhalika, Kondratenkov alisema Poland ni moja ya nchi zinazojaribu kuwa mwenyeji wa silaha za nyuklia za NATO, na kwamba wale wanaoilaumu Urusi kwa kukiuka sheria za Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki, IAEA wanapaswa kuthibitisha madai au “kubaki nayo wenyewe.”