Home Habari Kuu Upigaji kura waanza Afrika kusini ukiwashirikisha wapiga kura milioni 27

Upigaji kura waanza Afrika kusini ukiwashirikisha wapiga kura milioni 27

0

Upigaji kura umeanza nchini Afrika Kusini mapema Jumatano huku jumla ya wapiga kura milioni 27, wakitarajiwa kutekeleza haki za za kidemkrasia.

Utakuwa uchaguzi wa kwaza wenye ushindani mkali tangu taifa hilo lijinyakulie uhuru wake mwaka 1994 .

Vyama 70 vinawakilishwa katika zoezi hilo huku kukiwa pia na wagombezi wa kibinafsi 11, katika kiti cha Urais,Ubunge na waakilishi 9 wa mikoa.

Chama tawala cha ANC ambacho kilianzishwa na Rais wa kwanza hayati Nelson Mandela, aliyeikomboa nchi hiyo kutoka kwa utawala wa wakoloni na sera ya ubaguzi wa rangi, kinawania muhumula wa saba afisini.

Kura za maoni zimeashiria uwezekano wa chama cha ANC kinachoongozwa na Rais Cyril Ramaphosa, huenda kikalazimika kubuni serikali ya mseto kwani kitakosa kuwa na idadi kubwa ya wabunge.

Wapiga kura wakipiga foleni kupiga kura yao

Chama cha upinzani Democratic Alliance-DA, kimeunda muungano na vyama vingine 10 kama njia ya kutaka kuondoa ANC mamlakani

ANC ilipata asilimia 57.5 ya kura zote dhidi ya DA kwa asilimia 21 katika uchaguzi uliopita.

Idadi ya wanwake waliojisajili kuoiga kura ni asilimia 55 ikiwa milioni 15.

Kulingana na takwimu za tume ya uchaguzi nchini humo wengi wa wapiga kura waliojiandikisha, ni kati ya umri wa miaka 30 na 39 ambao kwa jumla ni milioni 26.7.

Hata hivyo takriban watu milioni 13.7 waliotimiza umri wa kupiga kura walikosa kujisajili ,milioni 8 kati ya idadi hiyo wakiwa chini ya umri wa miaka 30.

Kulingana na kura ya maoni huenda Rais Ramaphosa akakosa kufikisha asilimia 50, ya kura huku chama cha ANC kikitarajiwa kupoteza umaarufu wake kwa kiwango kikubwa.

Website | + posts