Home Kimataifa Upasuaji wa kwanza wa kutenganisha watoto wafanywa Tanzania

Upasuaji wa kwanza wa kutenganisha watoto wafanywa Tanzania

0
Watoto waliotenganishwa wakiwa na mama yao mzazi

Madaktari wataalamu wa upasuaji wazaliwa wa Tanzania wanaofanya kazi katika hospitali ya kitaifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam nchini Tanzania wamefanikiwa kutenganisha watoto mapacha.

Watoto hao walikuwa wameungana kwenye sehemu za tumbo na kifua na upasuaji huo ulichukua muda wa dakika 360 sawa na saa 6.

Msimamizi wa huduma za upasuaji katika hospitali hiyo Daktari Rachel Mhaville aliambatanisha kufanikiwa kwa upasuaji huo na uwekezaji wa kiwango kikubwa wa serikali.

Serikali hiyo ya awamu ya sita anasema imewekeza katika kununua vifaa muhimu vya kisasa vya hospitali na kuwekeza pia katika elimu ya madaktari.

Daktari Mhavile anasema fahari yao kubwa kando na kumaliza uoasuaji huo salama ni kwamba watekelezaji ni wazaliwa wa Tanzania.

Watoto waliotenganishwa wanaripotiwa kuendelea vizuri ambapo Daktari mwingine kwa jina Victor Ngota ambaye ni mtaalamu wa upasuaji wa watoto anaelezea kwamba walipokea watoto hao kwa mara ya kwanza Machi, 2023 punde baada ya kuzaliwa.

Baadaye walianzisha mpango mzima wa kuhusisha wataalamu mbali mbali kutathmini ubora wa afya ya watoto hao na jinsi watakua baada ya kutenganishwa kabla ya kutekeleza upasuaji.

“Ilituchukua muda wa takribani miezi 10 kupanga upasuaji wa watoto hawa.” alisema Daktari Ngota.

 

Website | + posts